Texas University Yaomba Kumsomesha Mtoto Wa George Floyd Bure

Mke Wa George Flod Na Mwanae
Muda mfupi tu baada ya Mwili wa baba yake kuzikwa huko Houston Texas, Chuo Cha Texas Southern University kimetangaza kumpa nafasi binti yake Gianna , ya kusoma chuoni hapo bure katika masomo yake yote ya elimu ya juu.

Kupitia kurasa zao za kijamii Texas University , wamethibitisha kuwa tayari wametoa ruhusa kwa binti Floyd kuja kujiunga na chuo hicho bure, endapo itampendeza.

George Floyd alizaliwa North Carolina, lakini alikulia na kusomea Houston Texas kabla ya kuhamia Minnesota ambapo umauti wake ulimkuta.

Ukiachana na ofa ya chuo hicho , Kanye west pia tayari ameshachangia zaidi ya Bilioni 4 za kitanzania kuhakikisha binti huyo anapata elimu nzuri.


EmoticonEmoticon