Trump Akataa Kubadili Majina Ya Kambi Za Kijeshi Kufwatia Maandamano Nchini Humo

Donld Trump
Rais wa Marekani Donld Trump anasema kwamba hatofikiria kubadilisha majina ya kambi za kijeshi zilizotajwa baada ya majenerali walioongoza jeshi la Marekani.
Alituma ujumbe wa twitter akisema kwamba kambi hizo ni miongoni mwa turathi kuu za Marekani.
Matamshi hayo ya bwana Trump yanajiri kufuatia ripoti kwamba maafisa wakuu wa jeshi walikuwa tayari kuruhusu mabadiliko kufuatia maandamano yaliosababishwa na kifo cha George Floyd.

 "Marekani iliwapatia mafunzo na kuwapeleka mashujaa wetu katika maeneo hayo ,na kufanikiwa kushinda vita viwili vya duniani. Hivyobasi utawala wangu hautafikiria kubadilisha majina ya kambi hizi na hata vifaa vya kijeshi.Historia yetu kama taifa lenye uwezo mkubwa duniani haitaingiliwa, Heshimuni jeshi letu.”Imeeleza Twita ya Donald Trump


EmoticonEmoticon