Ugonjwa Wa Corona Sasa Ni Tatizo Kuu Marekani

Marekani Corona
Daktari mkuu wa magonjwa ya kuambukizwa nchini Marekani Dkt Anthony Fauci anasema Marekani ina tatizo kubwa kwa kuwa maambukizi ya virusi vya corona imepanda kwa kasi katika majimbo 16.

Ndani ya miezi miwili alitoa ufafanuzi mfupi kwa wahudumu wa White House,Dkt Fauci alisema: "Namna nzuri ambayo tunaweza kukabiliana na janga hili ni kwa kushirikiana pamoja."
Kama mtaalamu wa afya alisema kuna mambo mengi ya kuyafanya ili kupunguza kasi ya maambukizi, makamu wa rais Mike Pence alisifia jitihada ambazo Marekani ilizichukua".
Zaidi ya maambukizi mapya 40,000 yalipatikana nchini Marekani siku ya Ijumaa.
Jumla ya maambukizi 40,173, ambayo yalitolewa na chuo kikuu cha Johns Hopkins, ilikuwa idadi kubwa kwa siku mpaka hapo, na rekodi ya maambukizi ilizidi kwa siku moja tu.
Marekani kuna zaidi ya maambukizi milioni 2.4 yaliothibitishwa na vifo zaidi ya 125,000 katika nchi nzima - idadi ambayo iko juu kuliko nchi nyingine.

Katika taarifa fupi aliyotoa siku ya Ijumaa, kikosi kazi cha White House waliwahimiza vijana pia kupima hata kama hawaoni dalili.
Bwana Pence alisema rais amekitaka kikosi kazi cha operesheni hii kuwaeleza Wamarekani kuwa kuna maambukizi mengi na kuna wagonjwa wengi wamelazwa hospitali katika majimbo ya kusini na Magharibi.
Jimbo la Texas, Florida na Arizona, mpango wa kufungua shughuli ziendelee umesitishwa kwa sababu ya kasi ya maambukizi.
Wakati maeneo mengine kesi za maambukizi zikiwa zinaongezeka kila kukicha na hivyo kufanya rekodi ya walioambukizwa kuongezeka pia.
Maafisa wa afya wa Marekani wanakadiria kuwa idadi ya maambukizi yaweza kuwa imeongezeka mara kumi zaidi ya ripoti iliyotangazwa.


EmoticonEmoticon