Wafanyakazi Wanne wa Ikulu Ya Rais Kenya Wamepatwa Na Corona

Rais Kenyata

Wafanyakazi wanne wa Ikulu ya rais nchini Kenya wamepatikana na virus vya corona.
Kwa mujibu wa msemaji wa Ikulu Kanze Dena, wafanyakazi hao waligunduliwa wameambukizwa COVID-19 baada ya kufanyiwa uchunguzi Alhamisi, Juni 11.
Maafisa hao walioambukizwa wamelazwa katika Hospitali ya rufaa ya Chuo Kikuu cha Kenyatta ambako wanaendelea kupata matibabu .
Msemaji wa Ikulu amewahakikishia Wakenya kuwa Rais Kenyata na familia yake wake wako salama na wamethibika kutokuwa na maambukizi ya corona.
''Ikulu inawafahamisha Wakenya kwamba rais na familia yake hawana ugonjwa wa Covid-19'', ilisema taarifa ya Bi Kanze Dena.
Taarifa hiyo pia iliwakumbusha Wakenya kwamba kila mtu yuko katika hatari ya kuambukizwa virusi vya corona.
Katika juhudi za kuzuia maambukizi ya Corona, wafanyakazi wote wanaoishi nje ya Ikulu pamoja na wageni wamedhibitiwa kwa kuzingatia mikakati iliyowekwa na wizara ya Afya.
Kufikia sasa Kenya ina jumla ya watu 3,727, walioambukizwa virusi vya corona kufuatia ongezeko la wagonjwa wengine wapya 133.
Credit:Bbc


EmoticonEmoticon