Wanaume Watatu Wakamatwa Kwa Kuwauza Watoto Wachanga Instagram

Mkuu wa polisi katika mji mkuu wa Iran -Tehran, Brigadia Jenera Hossein Rahimi, amesema kuwa mmoja wa watoto hao wachanga alikuwa ni wa siku 20. Mwingine alikua na umri wa mwezi mmoja.
Watoto hao wachanga walikua tayari wamenunuliwa kwa hadi dola $500 (£400), na walikua wanauzwa tena kwa dola kati ya $2,000 na $2,500.
Mmoja wa watu waliokamtwa anadaiwa kusema kuwa ''alikua anawapata watoto wachanga kutoka familia maskini " na "kuwakabidhi familia ambazo zinaweza kuwapatia maisha bora yajayo".
Brigadia Rahimi aliviambia vyombo vya habari vya Tehran kwamba maafisa wa polisi walifahamishwa juu ya "matangazo ya kibiashara katika mtandao wa Instagram yanayouza watoto wachanga".
Maafisa hao waligundua "kurasa 10 hadi 15 za aina hiyo" katika huduma ya kushirikisha picha na kubaini watoto wawili na wanaume watatu waliokua wamekamatwa, alisema. Watoto hao wachanga wamekabidhinwa kwa huduma za kijamii.


EmoticonEmoticon