Yoweri Museven Asema Serikali Yake Haitoshughulika Na Mwananchi Ambaye Atakufa Na Corona

Yoweri Museveni
Rais wa Uganda, 'Yoweri Museveni' amesema kuwa itakuwa ole wao kwa raia ambao watafariki dunia kutokana na ugonjwa wa corona kwani serikali yake haitawajibika.

Museveni aliwakashifu wananchi kwa kulegeza na hata wengine kupuuza masharti yaliowekwa na wizara ya afya ya kuzuia maambukizi ya virusi vya COVID-19.

Ingawa hakuna kifo kimeripotiwa nchini Uganda, visa vingi vya maambukizi vimeripotiwa siku za hivi karibuni.

” Watu wamekiuka amri ya kuvaa maski na wamepuuza sheria ya kutokaribiana, nikipita mjini naona watu wamerejelea maisha yao ya awali, wanajiambia kuwa hakuna mtu amefariki kutokana na ugonjwa huu, nataka kuwaambieni kuwa mtu akifariki dunia, hakuna ambacho hatujawaambia,” Museveni alisema.

Museveni amewataka wale wote ambao wamefungua biashara yao kuendele kuchukua tahadhari zinahitajika ili kuzuia maambukizi zaidi ya ugonjwa wa corona.

Kufikia sasa Uganda imerekodi visa 657 vya maambukizi ya virusi hivyo huku Kenya visa hivyo vikikaribia 3,000.
Credit:Radiojambo


EmoticonEmoticon