Zaidi Ya Watu Nusu Milioni Wamekufa Kwa Ugonjwa Wa Corona Duniani Kote

Corona marekani
Zaidi ya watu 500,000 duniani kote wamepoteza maisha yao kutokana na mlipuko wa virusi vya corona, kwa mujibu wa chuo kikuu cha Johns Hopkins University nchini Marekani.

Tangu mlipuko wa virusi hivyo nchini China mwishoni mwa mwaka jana, kumekuwa na wagonjwa zaidi ya milioni 10, kulingana na Johns Hopkins.
Nusu ya maambukizi yote yalikua yametokea nchini Marekani na Ulaya lakini sasa ugonjwa wa corona inaendelea kukua kwa kasi nchini Marekani.
Virusi hivyo vimeathiri Asia ya kusini na Afrika ambako kunatarajiwa kuwa na maambukizi mpaka mwishoni mwa Julai.
Mlipuko huo bado unaenea katika maeneo mengi ya dunia, kesi mpya zilizorekodiwa kwa siku sita zikiwa milioni moja.
Marekani imeripotiwa kuwa na jumla ya maambukizi milioni 2.5 na vifo 125,000 vilivyotokana na Covid-19 mpaka sasa na maambukizi zaidi katika nchi nyingine.

Majimbo ya Marekani ambayo yalikuwa yamefunguliwa wiki za karibuni haswa upande wa kusini , yameripotiwa kuwa maaambukizi yameongezeka.
Ongezeko la maambukizi mapya limeonekana zaidi huko Texas, Florida na majimbo mengine ambapo imewabidi kuweka tena zuio la biashara kuendelea.
Takwimu zinaonyesha mataifa kadhaa kutoka bara la Asia na waafrika wanaweza kupata maambukizi zaidi ya mataifa ya wazungu.
Nchi ambayo ni ya pili kuwa na wagonjwa wengi Brazil, taifa hilo lina wagonjwa milioni 1.3 na vifo vinavyozidi 57,000.


EmoticonEmoticon