Afrika Kusini Yafunga Shule Huku Idadi Ya Maambukizi Ya Corona Ikiendelea Kupanda

Afrika Kusini imefunga shule kwa wiki nne kuanzia Jumatatu kama sehemu ya kukabiliana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona.

Rais Cyril Ramaphosa amesema ilikuwa muhimu kuhakikisha shule hazigeuki kuwa vituo vya maambukizi wakati ambapo idadi ya wanaoathirika nchini humo inazidi kuongezeka kwa kasi ya juu mno duniani.
Shule za msingi na sekondari zilifunguliwa tena Julai 6.
"Kwa kuzingatia maoni ya washikadau na wataalamu mbalimbali, baraza la mawaziri limeamua kwamba shule zote za umma zitachukua mapumziko ya wiki nne," amesema Rais Ramaphosa.
Alisema kuwa mwaka wa sasa wa masomo utaongezwa hadi zaidi ya 2020 kwa sababu ya janga la corona.
"Tumechukua njia ya tahadhari kufunga shule kipindi hiki ambapo nchi inatarajiwa kupata maambukizi ya juu zaidi," alisema.


EmoticonEmoticon