Amerika Kusini Yaongoza Kwa Idadi Ya Maambukizi Ya Corona Duniani

Takwimu za shirika la habari la AFP zimeonyesha kuwa kiwango cha maambukizi ya virusi vya corona Amerika Kusini yameongezeka na kuizidi Amerika Kaskazini. 

Huku idadi ya maambukizi duniani yakiongezeka na kupita milioni 16 Amerika Kusini na visiwa vya Caribbean ndiyo maeneo yaliyoandikisha kiasi kikubwa cha walioambukizwa.

Kufikia sasa watu milioni 4.34 wameambukizwa virusi hivyo katika maeneo hayo kulingana na AFP. 

Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa maambukizi katika eneo hilo kuzidi Amerika Kaskazini ambapo Marekani ndiyo nchi iliyoathirika vibaya zaidi katika maambukizi na hata vifo.

Idadi jumla ya watu walioambukizwa virusi hivyo Marekani ni milioni 4.23. 

Huko Amerika Kusini Brazil ndiyo nchi iliyoathirika vibaya zaidi ikiwa na zaidi ya maambukizi milioni mbili na zaidi ya vifo 87,000.


EmoticonEmoticon