China Yasema Marekani Inataka Vita Mpya Baridi Na China

China marekani
Balozi wa China nchini Uingereza amesema kuwa Marekani inajaribu kuanzisha vita baridi mpya na taifa hilo la kikomunisti kwa sababu inatafuta kisingizio kuelekea uchaguzi wa rais mwezi Novemba.

Balozi huyo Liu Xiaoming, amesema siyo nchi yake iliyogeuka mbabe bali ni upande wa pili wa bahari ya Pacific unaotaka kuanzisha vita mpya baridi dhidi ya China, na hivyo wanalaazimika kujibu hilo.

Balozi huyo aliezungumza na waandishi habari, ameongeza kuwa China haina maslahi yoyote katika vita baridi, na wala haitaki vita vyovyote.

Amesema wameona kila kinachoendelea nchini Marekani, wakitaka kuitumia China kama kisingizio na kuilaumu kwa matatizo yao, na kwamba wanajua hii ni kwa sababu mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi.


EmoticonEmoticon