Bunge La Somalia Lamtimua Waziri Mkuu

Bunge la Somalia limepiga kura jana Jumamosi ya kumwondoa kwenye wadhifa wake Waziri Mkuu, Hassan Ali Khayre, ambaye ameendelea kusolewa kutokana na jinsi anavyoishughulikia hali ya usalama nchini humo.

Kwa mujibu wa spika wa Somalia, wabunge waliokubali hatua hiyo walikuwa 170 na  wanane walipinga.

Rais wa Somalia, Mohamed Abdullahi Mohamed, amesema katika taarifa kwamba anakubali uamuzi wa bunge kumtimua waziri mkuu ambapo atamteua waziri mkuu mpya hivi karibuni.


EmoticonEmoticon