Caf Yaahirisha Mashindano Ya Kandanda Barani Afrika

Afcon
Kinyang'anyiro cha Kombe la mataifa bingwa Afrika kilichotarajiwa kufanyika mwaka ujao 2021 kimeahirishwa hadi Januari 2022 na shirikisho la kandanda barani Afrika (Caf) kutokana na mlipuko wa virusi vya corona huku shindano kama hilo upande wa wanawake likifutiliwa mbali.

Shindano la wanaume lilitarajiwa kufanyika mwezi Januari mwaka ujao.
Katika habari nyingine, kinyang'anyiro cha kombe hilo miongoni mwa wachezaji wanaocheza barani Afrika CHAN ambalo lingechezwa mwezi Aprili sasa litafanyika Januari 2021.
Mashindano yote mawili yanatarajiwa kufanyika nchini Cameroon.
''Afya ndio kitu muhimu kwetu lazima tuwe macho'', rais wa Caf Ahmad Ahmad alisema katika mkutano na vyombo vya habari akitangaza uamuzi huo.
Hatua hiyo ina maana ya kwamba michuano hiyo inayofanyika mara mbili kwa mwaka sasa itafanyika mwaka mmoja na kombe la dunia la 2022 - kitu kilichofanyika mara ya mwisho mwaka 2010.


EmoticonEmoticon