Chanjo Ya Oxford Ilivyowezesha Mfumo Wa Kinga Mwilini Kukabiliana Na Virusi Vya Corona

Chanjo ya virusi vya corona iliyotengenezwa na Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza imeonekana kuwa ni salama na inachochea mfumo wa kinga ya mwili kukabiliana na virusi.

Majaribio ya chanjo hiyo yaliyowahusishwa watu 1,077 yameonyesha kuwa sindano ya chanjo hiyo waliyopigwa iliwezesha kutengeneza seli za protini za kinga ya mwili pamoja na seli nyeupe za damu zinazoratibu mfumo wa kinga ya mwili zenye uwezo wa kupambana na virusi vya corona, zinazofahamika kama T-cells.
Matokeo yanatia matumaini makubwa, lakini bado ni mapema sana kufahamu kama nana hii inatosha kuulinda mwili na majaribio makubwa yanaendelea.
Uingereza tayari imeagiza dozi milioni 100 za chanjo.


EmoticonEmoticon