CORONA : Kenya Yarekodi Visa Vipya Zaidi Ya 700 Kwa Saa 24

Kenya imerekodi wagonjwa wapya 788 wa virusi vya corona katika kipindi cha saa 24 zilizopita kutoka kwa sampuli 5,521, na hivyobasi kuongeza idadi ya wagonjwa waliothibitishwa na ugonjwa huo kukaribia 20,000.

Idadi hiyo ambayo ni ya juu zaidi kuripotiwa imeongeza jumla ya wagonjwa kufikia 19,913.
Akitoa tangazo hilo siku ya Alhamisi katibu tawala katika wizara ya Afya Rashid Aman pia alifichua kwamba wagonjwa wengine 14 wamefariki kutokana na Covid 19, na kufanya idadi ya waliofariki kutokana na maradhi hayo kufikia 325.
Wagonjwa wengine 100 wameripotiwa kupona na hivyobasi kuweka idadi ya waliopona kufikia 8,121.
Credit:Bbc


EmoticonEmoticon