CORONA : Kenya Yasajili Visa Vipya 497 Kwa Siku Moja Jumla 10,791

Mercy Mwangangi
Kenya siku ya jana (Julai 14) imesajili visa vipya 497 vya corona na kufikisha idadi ya jumla ya waliopatwa ugonjwa huo kuwa 10,791 .

Visa hivyo ni kutoka sampuli  4922  amesema katibu wa utawala wa wizara ya afya  Mercy Mwangangi.

” Idadi hii itazidi kuongezeka na hili linafaa kutupa wasiwasi. Nairobi inazidi kuongoza kwa idadi ya watu  waliopata ugonjwa  baada ya visa 518 kusajiliwa jijini katika siku tatu zilizopita.
” Wakaazi wa jiji wanafaa kuwa na tahadhari ‘ amesema Mwangangi.

Mwangagi pia ametoa rai kwa wakenya kukoma kuendeleza unyanyapaa dhidi ya watu walio na ugonjwa huo .
Credit:Radiojambo


EmoticonEmoticon