CORONA : Marekani Yarekodi Visa Vya Juu Zaidi Ya 65,000 Kwa Siku Moja

Corona Hospital
Marekani imeweka rekodi nyingine mpya wa maambukizi mengi ya corona. 

Kulingana na takwimu za chuo kikuu cha Johns Hopkins, watu 67,000 wamethibitishwa kuambukizwa kwa siku moja.

Marekani ambayo ndiyo nchi inayoongoza ulimwenguni kote kwa idadi ya walioambukizwa virusi hivyo, imekuwa ikirekodi maambukizi ya juu tangu mwisho wa mwezi Juni, haswa kusini na magharibi mwa nchi hiyo.

Kwa siku 10 zilizopita, idadi ya watu wapya ambao wamekuwa wakiambukizwa nchini humo, wamekuwa kati ya 55,000 hadi 65,000 kila siku.


EmoticonEmoticon