CORONA : Shirika La Afya Duniani Latoa Onyo Kwa Mataifa

WHO
Janga la corona litakuwa ''baya na baya zaidi'' ikiwa serikali zitashindwa kuchukua hatua madhubuti, Shirika la afya duniani (WHO) limetahadharisha.

Mkuu wa shirika hilo Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema ''nchi nyingi sana (zilikua) zikielekea kwenye njia isiyo sahihi.''
''Idadi ya watu walioambukizwa ilikuwa ikiongezeka kwenye maeneo ambayo masharti yalikuwa hayafuatwi'', aliongeza.
Katika mkutano wa siku ya Jumatatu , Dkt Tedros amesema ''ujumbe mchanganyiko kutoka kwa viongozi'' umekuwa ukishusha uaminifu wa Umma katika jitihada za kudhibiti janga la virusi vya corona.

''Virusi vinaendelea kuwa adui wa kwanza wa watu, lakini hatua za serikali nyingi na watu hazioneshi hilo,'' alisema.
Dkt Tedros amesema kuwa hatua kama vile ya kukaa mbali na mwingine, kunawa mikono na kuvaa barakoa katika mazingira yanayolazimu kufanya hivyo zilipaswa kuzingatiwa kwa kiasi kikubwa, akitahadharisha kuwa kutakuwa na ''hakuna kurejea kwenye maisha ya zamani siku za usoni''.
''Ikiwa vitu vya msingi havifuatwi, kuna njia moja janga hili litaelekea,'' dkt aliongeza: ''hali itakuwa mbaya na mbaya sana.''


EmoticonEmoticon