CORONA : Siri Ya Vile Popo Wanavyoweza Kuishi Na Virusi Yafichuliwa

Popo

Wanasayansi wanasema wamechunguza vinasaba vya popo sita duniani.
Maisha yao yanajumuisha kidokezo cha vinasaba vyao vinavyowafanya kuwa na kinga ya kipekee inayowalinda dhidi ya virusi vya corona.
Watafiti wana matumaini kwamba taarifa hizo zitawasaidia kufahamu siri ya vile popo wanabeba virusi vya corona na kuvisambaza bila wao wenyewe kupata maambukizi.
Wanasema kuwa huenda hilo likatoa suluhu ya kudumu kusaidia afya ya mwanadamu wakati wa janga hili na hata siku za usoni.
Profesa Emma Teeling kutoka chuo cha Dublin amesema kuwa chembe za urithi walizochunguza zimewafanya kubaini kwamba popo wana mifumo maalum ya kinga.
Na kuelewa vile popo wanavyoweza kumudu virusi vya corona bila wao kupata maambukizi kunaweza kusaidia kupata tiba mpya ya ugonjwa wa Covid-19.
"Ikiwa tunaweza kuiga kinga ya popo dhidi ya virusi, unaweza kupata tiba," ameiambia BBC News.
"Tayari imeshabadilika na kukua, kwahivyo sio kwamba uvumbuzi unaanza mwanzo. Sasa tuna vifaa vya kutuwezesha kuelewa hatua tunazohitajika kuchukua; tunahitajika kuvumbua dawa ili kufanikiwa."


EmoticonEmoticon