Dawa Ya Kutibu Na Kumaliza Kabisa Kikohozi Kwa Muda Mfupi

Karafuu
Karafuu hutumika kama kiungo na pia ni dawa muhimu kwa binadamu. 
Ina uwezo wa kukusaidia magonjwa mengi lkiwemo tumbo, misuli na meno.

Ponda karafuu sita changanya na asali katika kijiko cha mezani kisha gawa mchanganyiko huo katika makundi mawili yanayolingana, ongeza chumvi kidogo katika kila moja.

Lamba taratibu mchanganyiko huo kutwa mara mbili kama yalivyo makundi hayo kwa maana ya asubuhi moja na jioni jingine. Endelea katika kipindi cha siku tatu hadi saba utaondokana na tatizo la kikohozi.

Mara nyingi kikohozi kinaweza kusababishwa na mabadiliko ya hewa au majira au kuziba mifereji ya kupitisha hewa ndani ya mapafu.

Kikohozi kinapotokea lengo ni kuondoa chembechembe zisizohitajika katika njia ya kupitisha hewa. Kikohozi cha kawaida kinaweza kupona kabisa iwapo utazingatia maelekezo ya hapo juu.


EmoticonEmoticon