Habari Kubwa Za Soka Ulaya Alhamisi Julai 16

Kalidou Koulibaly
Tetesi Za Soka Ulaya Alhamisi Julai 16

1. Manchester City wametakiwa kuweka mezani kitita cha pauni milioni 65 kwa ajili ya beki wa Napoli Kalidou Koulibaly ,29, ambaye anauhishwa na taarifa za kuhamia Liverpool na Manchester United na awali alikuwa na thamani ya pauni milioni 80.

2. Manchester City inamtazama mshambuliaji wa Inter Milan Muajentina Lautaro Martinez,22, kama mchezaji muhimu katika kuchukua nafasi ya Sergio Aguero,32.
Hatahivyo, Martinez yuko ukingoni kumalizana na hatua za uhamisho kuelekea Barcelona.
3. Bayern Munich inatafuta pauni milioni 40 kwa ajili ya kiungo wao wa kati wa zamani Thiago Alcantare, Mhispania ,29. 
Bayern wanafikiriwa kujitoa katika kinyang'anyiro cha kumnasa kiungo Kai Havertz,21 anayekipiga na Bayer Leverkusen.

4. Everton, Atletico Madrid na Bayern Munich wanatarajiwa kuweka nia ya kumnyakua winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha msimu huu, huku Newcastle pia ikimfuatilia kwa karibu mchezaji huyo,27.
5. Southampton wana matumaini ya kupata mkataba wa kudumu wa pauni milioni 10 kwa ajili ya mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Totteham, Muingereza Kyle Walker-Peters,23, ambaye anakipiga Saints kwa mkopo tangu mwezi Januari


EmoticonEmoticon