Habari Kubwa Za Soka Ulaya Alhamisi Julai 23

Tetesi Za Soka Ulaya
Tetesi Za Soka Ulaya Alhamisi Julai 23

1. Arsenal wanajiandaa kumpatia mkataba mpya mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 31, unaokadiriwa kuwa £250,000 kwa wiki pamoja na marupurupu mengine katika juhudi za kumshawishi asiondoke klabu hiyo. 
2. Mkufunzi wa Rangers Steven Gerrard, 40, amekata ofa ya kuwa meneja mpya wa klabu ya Bristol City.
3. Valencia wanajiandaa kumnunua kipa wa Chelsea na Uhispania Kepa Arrizabalaga, 25, pamoja na mchezaji nyota wa Manchester City Mhispania David Silva, 34.
4. Borussia Dortmund wameanza mchakato wa kumsaka winga wa Werder Bremen na Kosovo Milot Rashica, 24, huku wakimtafuta atakayejaza pengo litakaloachwana mshambuliaji wa England Jadon Sancho, 20, ambaye amehusishwa na uhamisho wa kwenda Manchester United.
5. Winga wa Bayern Munich Leroy Sane, 24, amemsihi beki wa Austria David Alaba, 28, kusalia katika klabu hiyo badala kurejea tena katika klabu yake ya zamani Manchester City, ama kwenda Real Madrid. 


EmoticonEmoticon