Habari Kubwa Za Soka Ulaya Alhamisi Julai 30

Tetesi Za Soka Ulaya Alhamisi Julai 30

1. Kocha wa Tottenham Hotspur Jose Mourinho anataka kumsajili winga anayekipiga Porto, raia wa Colombia Luis Diaz, 23.

2. Inter Miami, inayomilikiwa na nahodha wa zamani wa England David Beckham, ina mpango wa kumfanya mshambuliaji wa Barcelona Luiz Suarez kuwa chaguo lao la kwanza kubwa la usajili.
3. Wakala wa mchezaji anayetolewa macho na Manchester City na Paris St-Germain David Alaba, ameitaka Bayern Munich kumlipa mchezaji beki huyo wa kushoto, 28, pauni milioni 18 kuongeza mkataba wake.

4. West Ham United wana mpango na mchezaji wa Queens Park Rangers, Ryan Manning, 24.
5. Mazungumzo kati ya Manchester United na mlinda mlango wa Kiingereza Dean Henderson, 23- ambaye ametumia msimu wake akichezea Sheffield United kwa mkopo- yamekuwa kwenye hatua muhimu baada ya kufanyika kwa majuma kadhaa.


EmoticonEmoticon