Habari Kubwa Za Soka Ulaya Ijumaa Julai 17

Paul Pogba
Tetesi Za Soka Ulaya Ijumaa Julai 17

1. Kiungo Mfaransa Paul Pogba, 27 , yuko karibu kukubali mkataba mpya wa miaka mitano kuichezea Manchester United.

2. Bayer Leverkusen wamekubali kuwa kiungo wa kati Mjerumani Kai Havertz, 21, amechagua kujiunga na Chelsea lakini klabu hiyo inataka kuusogeza mbele uhamisho mpaka mwishoni mwa mwezi Agosti.
3. Arsenal iko mbioni kumsajili beki Mfaransa Malang Sarr, lakini mchezaji huyo, 21, anayepatikana kwa uhamisho wa bila malipo akitokea Nice tayari ameshafuatiliwa na vilabu vya Italia na Ujerumani.

4. Manchester United imekubali kuingia mkataba na beki wa kushoto wa Real Madrid, Alvaro Fernandez Carreras, 17, ambaye atatia saini mkataba wa miaka minne kukipiga Old Trafford.
5. Kocha wa zamani wa Southampton na Tottenham Mauricio Pochettino yuko kwenye orodha ya Inter Milan na Juventus ikiwa vilabu hivyo vya Italia vitawafuta kazi makocha wa zamani wa Chelsea - Antonio Conte na Maurizio Sarri - mwishoni mwa msimu. 


EmoticonEmoticon