Habari Kubwa Za Soka Ulaya Ijumaa Julai 24

Tetesi Za Soka Ulaya Ijumaa Julai 24
Tetesi Za Soka Ulaya Ijumaa Julai 24

1. Benfica imesitisha azma yake ya kumsaka mshambuliaji Edinson Cavani, 33, huku mchezaji huyo aliyekuwa Paris St-Germain akidai karibu pauni milioni 18 kwa kila msimu.

2. Chelsea imekuwa ikimfuatilia mlinzi wa Atletico Madrid na Uruguay Jose Gimenez, 25, huku kocha Frank Lampard akiwa anafuatilia kutatua mapungufu ya upande wa ulinzi wa kikosi chake. 
3. Leroy Sane, 24, alionekana kuthibitisha wakati anatambulishwa Bayern Munich kwamba mchezaji mwenzake wa Ujerumani Kai Havertz, 21, ianaelekea Chelsea kutoka Bayer Leverkusen msimu huu.

4. Jesse Lingard, 27, amemtaka kiungo wa kati raia mwenzake wa Uingereza Jadon Sancho, 20, kuondoka Borussia Dortmund na kujiunga naye Manchester United msimu huu. 
Sancho ni mmoja kati ya wachezaji watano ambao kocha wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer anataka wajiunge na kikosi chake. Hata hivyo huenda akalazimika kuuza baadhi ya wachezaji ili kupata pesa.

5. Ligi ya Serie A nchini Italia imethibitisha kwamba inafanya mazungumza ya kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester City na Liverpool Mario Balotelli. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia, 29 anaondoka kalbu yake ya sasa Brescia.


EmoticonEmoticon