Habari Kubwa Za Soka Ulaya Jumanne Julai 21

Pochettino na Sarri
Tetesi Za Soka Ulaya Jumanne Julai 21

1. Juventus wanatafakari uwezekano wa kumnunua mkufunzi wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino kuchukua nafasi ya Maurizio Sarri kama kocha wao mpya.

2. Manchester United wanatarajiwa kuwasilisha ofa ya £80m kwa Borussia Dortmund kumnunua winga wa England Jadon Sancho, 20.

3. Chelsea wanazungumza na Bayer Leverkusen kuhusu mkataba wa £70m kumsajili Kai Havertz, baada ya klabu zote zilizokuwa zikimng'ang'ania kiungo huyo wa Ujerumani aliye na miaka 21 zikijiondoa katika kinyang'anyiro hicho.

4. Kiungo wa kati wa Arsenal Mjerumani Mesut Ozil, 31, amekataa ofa ya kujiunga na Fenerbahce inayoshiriki ligi kuu ya Uturuki .Lakini Ozil huenda akajiunga na ligi hiyo, Istanbul Basaksehir inasemekana iko tayari kumnunua.

5. Arsenal huenda wakaondoa masharti ya kulipa £40m katika mkataba wa mshambuliaji wa Sporting Joelson Fernandes ,17 katika kipindi cha saa 24 zijazo.
Licha ya dau lao kukataliwa, Tottenham wanamatumaini kuwa watakmilisha mchakato wa kumsajili beki wa Beijing Guoan na Korea Kusini Kim Min-jae, ambaye amepewa jina la 'Virgil van Dijk wa Korea Kusini'.


EmoticonEmoticon