Habari Kubwa Za Soka Ulaya Jumanne Julai 28

Sancho, Coutinho
Tetesi Za Soka Ulaya Jumanne Julai 28

1. Manchester United waliandaa ofa ya kwanza ya Pauni milioni 89 ili kumpata Winga Jadon Sancho ambayo imekataliwa na Borrusia Dotmund.

Klabu hiyo bado haijawasilisha zabuni kwa ajili ya Sancho pamoja na kwamba Dortmund inahitaji pauni milioni 110 kiasi ambacho ni kiasi kikubwa cha pesa, lakini inaaminika kuwa mazungumzo yataweza kuwafikisha kwenye makubaliano.
2. Chelsea imeanza mazungumzo na Bayer Leverkusen kwa ajili ya winga Mjerumani Kai Havertz, 21.

3. Winga wa Brazil Willian ,31, anaweza kukubali mkataba mpya na Chelsea mwishoni mwa wiki baada ya mazungumzo baina ya pande mbili.

4. Kiungo mchezeshaji anayekipiga Barcelona Philippe Coutinho ameiomba Arsenal muda zaidi kufanya maamuzi kuhusu mustakabali wake, huku Leicester City na Tottenham pia wakiwa wanamtolea macho Mbrazili huyo, 28.

5. Manchester City wanajiandaa kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Wales Cameron Coxe, 21 kwa uhamisho huru, baada ya kuachiwa na Cardiff City.


EmoticonEmoticon