Habari Kubwa Za Soka Ulaya Jumatano Julai 1

Jadon Sancho
Tetesi Za Soka Ulaya Jumatano Julai 1

1. Manchester United haitalipa zaidi ya pauni milioni 50 kwa winga wa Borussia Dortmund Jadon Sancho. Hatahivyo, klabu hiyo ya Bundesliga inataka ongezeko la pauni milioni 100 kwa ajili ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20.

2. Manchester City wana mpango wa kumsajili mchezaji wa nafasi ya ulinzi anayekipiga katika klabu ya Bournemouth Nathan Ake, 25. Hatahivyo wanaweza kukabiliana na ushindani kutoka Chelsea, ambao wanamtaka mchezaji huyo pia.

3. Beki wa kulia wa Barcelona Marc Jurado,16, ameondoka katika klabu ya Catalan. Mhispania huyo anajiandaa kujiunga na Manchester United msimu huu.

4. Juventus imeongeza ushawishi wao kwa winga Mhispania anayechezea Valencia Ferran Torres,20. Mchezaji huyo amekuwa akihusishwa na tetesi za kuhamia Manchester United na Borussia Dortmund. 

5. Mchezaji wa nafasi ya ulinzi wa Real Madrid Achraf Hakimi, 21,ameonekana Italia kabla ya uhamisho wa pauni milioni 36 kwenda Inter Milan. 


EmoticonEmoticon