Habari Kubwa Za Soka Ulaya Jumatano Julai 15

Neymar, Coutinho, Mbappe
Tetesi Za Soka Ulaya Jumatano Julai 15

1. Real Madrid inaamini kuwa mshambuliaji Kylian Mbappe ,21, atakuwa na mazungumzo nao kuhusu uhamisho kutoka Paris St-Germain.

2. Barcelona inamuuza kiungo mchezeshaji wa Brazil Philippe Coutinho, 28, kwa Arsenal na Newcastle huku wakijaribu kutafuta fedha za kumnunua mshambuliaji wa Inter Milan na Argentina Lautaro Martinez, 22.

3. Chelsea iko tayari kumpatia kipa wa Atletico Madrid na Slovenia Jan Oblak ofa £90.7m.

4. Mshambuliaji wa Brazil Neymar, 28, anataka kurudi Barcelona, na Paris St-Germain wanapiga hesabu za thamani yake huku akiwa amesalia na kandarasi ya miaka miwili katika mkataba wake.

5. Manchester United itakosa malipo ya £25m kutoka kwa wafadhili iwapo watafeli kufuzu katika michuano ya kombe la klabu bingwa Ulaya.


EmoticonEmoticon