Habari Kubwa Za Soka Ulaya Jumatano Julai 22

Tetesi Za Soka Ulaya Jumatano Julai 22

1. Mshambuliaji wa Aston Villa raia wa Tanzania Mbwana Samatta, 27, huenda akaelekea Fenerbahce baada ya kushindwa kuiridhisha Villa Park tangu alipojiuga nao Januari. 

2. Chelsea imejitayarisha kutoa ofa kwa mlinda lango mwingereza Dean Henderson, 23, ya pauni 170,000 kwa wiki ambaye sasa hivi yuko Sheffield United kwa mkopo , kujaribu kumshawishi kujiunga nao kutoka Manchester United.

3. Henderson atatafuta kwa kila namna kuondoka tena kwa mkopo labda tu apate hakikisho kutoka Manchester United kwamba atapata fursa ya kushindana na mlinda lango wa Uhispania David de Gea, 29, awe chaguo la kwanza.

4. Chelsea pia itajitahidi kusaini mkataba na mlinda lango wa Barcelona na Ujerumani Marc-Andre ter Stegen, 28, na iko tayari kutoa ofa kwa mlinda lango wa kimataifa Kepa Arrizabalaga, 25, kama sehemu ya makubaliano yoyote yale.

5. Kocha wa Arsenal Mikel Arteta ana uhakika kwamba mshambuliaji wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 31, atasaini mkataba mpya na klabu hiyo.


EmoticonEmoticon