Habari Kubwa Za Soka Ulaya Jumatatu Julai 27

Mikel Arteta
Tetesi Za Soka Ulaya Jumatatu Julai 27

1. Kiungo wa kati wa Southampton James Ward-Prowse,25, amekubali dili jipya ambalo litamfanya kusalia na kabu hiyo mpaka mwaka 2025.

2. Winga wa Leicester City na timu ya taifa ya England kwa wachezaji wa chini ya miaka 21, Harvey Barnes, anawindwa kusajiliwa na Liverpool.
3. Liverpool pia imemfuatilia beki wa kati wa Schalke na Mturuki Ozan Kabak, ambaye awali alikuwa akiwavutia Manchester City, Juventus na Barussia Dortmund.
4. Borussia Dortmund wameanza mazungumzo kwa ajili ya kiungo mshambuliaji wa Lille, Mfaransa Jonathan Ikone, 22, wakimfanya kuwa mbadala wa winga Jadon Sancho,20, ambaye amekuwa akihusishwa na taarifa za kuhamia Manchester United.

5. Kocha wa Arsenal Mikel Arteta amedokeza kuwa anaweza kuingia kwenye soko la usajili kutokana na jeraha la mchezaji wa nafasi ya ulinzi, Mjerumani Shkodran Mustafi,28, hali ambayo imemfanya kuwa na upungufu wa wachezaji wa safu ya ulinzi. 


EmoticonEmoticon