Habari Kubwa Za Soka Ulaya Ijumaa Julai 31

Gareth Bale, Jadon Sancho
Tetesi Za Soka Ulaya Ijumaa Julai 31

1. Uhamisho unaokisiwa wa Jadon Sancho kwenda Manchester United uko karibuni kufikiwa, wakati Borussia Dortmund wakiwa tayari kukubali ada ya awali ya pauni milioni 60 kwa ajili ya winga huyo, 20.

2. Mshambuliaji wa Mexico Raul Jimenez, 29, yuko njiani kuelekea Manchester United baada ya Wolves kukubali ada ya pauni milioni 27 kumsajili mshambuliaji wa Braga, Mreno Paulinho.
3. Chelsea imeweka mezani ofa kwa ajili ya mlinda mlango wa Barcelona Marc-Andre ter Stegen, 28. 
4. Gareth Bale, 31, amemwambia kocha wa Wales Ryan Giggs kuwa ana dhamira ya kusalia Real Madrid msimu ujao. hata kama kukosa michezo kutaathiri kipato chake.

5. Chelsea na Manchester City ni miongoni mwa vilabu vinavyoongoza ambavyo vinafuatilia kama mchezaji David Alaba, 28, atasaini mkataba mpya na Bayern Munich.


EmoticonEmoticon