Hawa Ndyo Wapenzi Waliofunga Ndoa Msituni Huko Mipakani

Bibi harusi mmoja kutoka Norway na mpenzi wake kutoka Sweden waliandaa sherehe ya harusi yao kwenye mpaka kati ya mataifa hayo.

Katika sherehe hiyo ya kipekee, wageni waalikwa walisimama kila upande wa mpaka, kuambatana na sheria za kudhibiti ugonjwa wa Covid-19.
Wanandoa hao waliiambia BBC kwamba wasingeweza kustahimili upweke na kungojea muda zaidi ili vikwazo viondolewe.
''Hatukutaka kamwe kubadilisha tarehe yetu ya harusi ... tulichotaka tu ni ndoa yetu! ''.
Na kwa sababu Sweden ilikataa kuweka vikwazo na makataa ya kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa Covid19, baadhi ya mataifa jirani kama Norway hayajaridhishwa na mbinu walioitumia na hivyo hazijajumuisha nchi hiyo kwenye orodha ya mataifa ambayo raia wake wanaweza kuingia na kutoka.
Kutokana na hali hiyo, walibadilisha pete zao katikati ya msitu katika mkoa wa Holebekk ulioko Kusini Mashariki mwa Norway karibu na mpaka wa Sweden.
Walisimama upande mmoja wa mpaka, wakitengwa na uzio wa utepe mweupe mbali na familia na marafiki wao.
Wasaidizi wao pia walitengwa na utepe mweupe .
Bi harusi, Camilla Oyjord, alisema kuwa alipendekeza wazo hilo kama utani tu, lakini kinyume na matarajio yake marafiki na familia yake wakalishabikia kwa hamasa kubwa.
'' Tulitaka kuwa mume na mke! Upendo una nguvu sana unaweza kushinda changamoto zote! '' alisema.
Bwana harusi, Alexander Clern, kwa upande wake anasema hawakudhania wangepata mashahidi kwani ilikuwa ni mwendo mrefu mnondani ya msitu, lakini walifurahishwa na idadi kubwa ya wageni waalikwa waliohudhuria harusi yao.
Aidha harusi yao pia ilikuwa na wageni wawili ambao hawakualikwa - maafisa wa polisi ambao walikuwa huko ili kuhakikisha hakuna mtu anakiuka umbali wa mtu hadi mwingine.
'' Maafisa hao wa polisi walituuliza kwa heshima ikiwa wanaweza kuhudhuria harusi yetu kutazama. Tulikubali, '' Maharusi hao waliongezea.
Maharusi hao walishtushwa na idadi ya wageni walijitokeza kuhudhuria haru yao ya kipekee.


EmoticonEmoticon