Imesemekana Drake Akijitegemea Atakuwa Msanii Tajiri Sana Ambaye Haijawahi Kutokea Kwenye Historia

Drake
Drake alitangaza kuwa album yake ijayo haitakuwa chini ya usimamizi wa label ya Cash Money Records.

Sasa kwa mujibu wa Steve Stoute, mkongwe katika biashara ya muziki amesema Drake atakuwa msanii mwenye pesa nyingi kwenye historia ya muziki kama akiwa msanii wa kujitegemea kwa sababu atakuwa akichukua mapato yote ya kazi yake.

"Nilisema hii awali, Drake atabadilika kwenye miezi sita ijayo, ataingiza pesa nyingi sana kwenye historia ya biashara ya muziki. Kampuni zote hazitaki hilo litokee, kwa sababu siku ikitokea, wanaweza pia kufunga biashara zao." alisema Steve.

Kama Drake akiachana na label inayomsimamia ambayo huchukua asilimia kwenye mapato yake ya muziki basi biashara yote ya muziki itakuwa kichwani mwake

"Kama Drake akijitegemea, biashara ya muziki itafikia mwisho. Kama Drake akijitegemea, biashara ya muziki itakufa kwa sababu atatengeneza mamilioni ya pesa." aliendelea kukazia Steve. 

Drake ambaye kwa sasa amesainiwa na Cash Money kupitia Universal Music Group inayomilikiwa na Republic Records.


EmoticonEmoticon