India Yanunua Ndege Za kivita Huku Wasiwasi Kati Yake Na China Ukizidi Kuongezeka

Jeshi la India limepokea ndege tano za kivita aina ya Rafale huku kukiwa na wasiwasi mkubwa kati yake na China.

Ndege hizo ni miongoni mwa makubaliano ya taifa hilo na lile la Ufaransa yaliofanyika mwaka 2016 kununua ndege 36.
Delhi inatumai kuimarisha jeshi lake la angani linalotumia ndege za zamani za kisoviet kupitia nununuzi dege hizo mpya.
lakini watalaamu wanaonya kwamba ndege hizi haziwezi kutumika moja kwa moja iwapo kutakuwa na vita.
Mwanaanga mstaafu Pranab Barbora, ambaye alisimamia ununuzi wa ndege za kivita aina ya jaguar aliambia BBC kwamba kuwasili kwa Rafale ni hatua nzuri kwasasabu itaimarisha uwezo wa jeshi la angani.
''Lakini itachukua muda kabla ya ndege hizi kufanza kufanya kazi . Lazima uweke msururu wa kimkakati, kuwafunza mafundi na wafanyakazi wa ardini nchini India'', alisema.
Aliongezea kwamba inachukua hadi miaka miwili kabla ya kikosi kipya kuanza operesheni.
Kikosi hicho cha Rafale kitaanza kufanya kazi kitakapomiliki takriban ndege 18. Kuwasili kwa ndege nyengine kunatarajiwa kukamilika mwaka ujao.


EmoticonEmoticon