iPhone, Samsung Kutoka Bila Charger Ya Kuchajia Simu Hizo Kwa Toleo Jipya

iPhone, Samsung
Siku za karibuni kumekuwa na ripoti ambazo zinadai kuwa kampuni kubwa za kutengeneza simu za Apple na Samsung hivi karibuni zitakuwa zinatoa simu zake bila kuwepo kwa chaja, earphone wala waya wa USB ndani ya box.

Inasemekana kampuni ya Apple inatarajia kuzindua simu mpya za iPhone 12 bila kuwepo kwa chaja wala waya ndani ya box. Hata hivyo mbali ya chaja na waya, ripoti hizo zinadai kuwa simu hizo mpya pia zitakua hazina earphone ambazo zimekuwa zikija kwenye box pale unapo nunua simu mpya iPhone.

Ripoti mpya zimesambaa mtandaoni zikiwa zinadai kuwa kampuni ya Samsung nayo inatarajia kuanza kuuza simu zake bila kuwepo kwa chaja kwenye box kuanzia mwaka 2021.

Hata hivyo inadaiwa kuwa, hatua hizi zinakuja kutokana na kuwepo kwa chaja nyingi duniani kiasi cha kuchafua mazingira hivyo hatu hii inakusudi la kutunza mazingira.

Chaja, earphone na waya wa USB vyote vinategemewa kuuzwa kwa bei tofauti pale mteja atakapokuwa anahitaji.

Mbali na hali hii kuleta hamaki kwa watu mbalimbali, lakini pia inasemekana kuwa sababu hii ya kutokwepo kwa chaja kwenye box kutafanya simu kuuzwa kwa bei nafuu kutokana na kupungua kwa gharama za usafirishaji ambazo ukokotolewa kwa kuangalia uzito wa bidhaa usika.

Hata hivyo zipo ripoti ambazo zinadai kuwa simu za iPhone 12 zinatarajiwa kuja zikiwa zinauzwa kwa bei nafuu zaidi huku ikidhaniwa kuwa moja ya sababu ikiwa ni hii ya kutokwepo kwa chaja ndani ya box.

Kwa sasa hizi bado ni tetesi na huenda taarifa kamili kuhusu hii tukazipata siku za karibuni wakati Apple ikizindua simu zake mpya za iPhone 12. 

Kama Apple wakifanya hivi basi ni wazi kuwa lazima na kampuni ya Samsung itafuata huku tukisubiri na kampuni nyingine kujiunga kwenye msafara huu


EmoticonEmoticon