Iran Yaiwashia Moto Marekani, Yashambulia Meli Yake Kwa Mabomu Makali

Iran imeshambulia kwa makombora makali meli bandia ya kivita ya Marekani katika mlango bahari wa kimkakati wa Hormuz.

Zoezi hilo lilishirikisha mashambulio makali hatua iliofanya kambi mbili za Marekani kujiweka katika hali ya tahadhari.
Jeshi la Marekani lilishutumu tabia hiyo mbaya iliotekelezwa na Iran ikiitaja kama jaribio la kutishia na kichokozi.

Zoezi hilo linajiri wakati ambapo kuna hali ya wasiwasi kati ya Tehran na Washington katika eneo la Ghuba.
Maelezo ya picha,Wanajeshi wa Iran walirusha makombora wakilenga meli ya Marekani.

Meli hiyo ya kivita inayofanana na ile ya Marekani ambayo mara nyingi hutumiwa kubeba ndege za kivita inaonekana ikiwa imebeba ndege bandia ikiingia katika eneo la Ghuba.

Makombora baadaye yanarushwa kutoka maeneo tofauti ikiwemo mengine ambayo yanailenga meli hiyo.


EmoticonEmoticon