Kanye West Azindua Kampeni Rasmi Za Uchaguzi Kuwania Kiti Cha Uraisi Wa Marekani

Kanye West
Kanye West amezindua rasmi kampeni yake kwa ajili ya uchaguzi wa urais Marekani 2020, kwa kufanya mkutano wa kampeni huko Charleston, South Carolina ambao haukukubalika.

West, 43, anawania urais kama mgombea kupitia chama chake cha "Birthday Party".
Katika mkutano huo, mwanamuziki huyo wa mtindo wa kufoka foka alionekana kufanya maamuzi ya kusthukiza ya kisera na kuonekana kuzungumzia masuala kadhaa ikiwemo uavyaji mimba na mwanahakati anayependelea uavyaji mimba Harriet Tubman.
Mashabiki wanahoji ikiwa kujiingiza kwenye kinyang'anyiro cha kuingia Ikulu ya White House ni njia ya kujitafutia umaarufu.
Katika mkutano wa Charleston hakuonesha kuwa kujitoa kwake katika kampeni ni kwa kumaanisha. Lakini katika ujumbe ambao sasa hivi umeondolewa katika akaunti ya Twitter ya West alioandika Jumamosi, ulionesha nyimbo za albamu anayotaka kutoa, jambo ambalo limeongeza maswali.
Wakati mmoja alianza kulia alipokuwa anazungumzia suala la uavyaji mimba, akisema wazazi wake karibu tu watoe mimba yake: "Leo hii hakungekuwa na Kanye West, kwasababu baba yangu alikuwa na shughuli nyingi."
Aliongeza: "Kidogo tu nimuue binti yangu... hata kama mke wangu [Kim Kardashian West] angenipa talaka baada ya hotuba hii, alimleta North hapa duniani, hata kama sikuwa tayari."
Kanye West
Hata hivyo aliongeza kwamba anaamini kuwa uavyaji wa mimba unastahili kuendelea kukubalika kisheria lakini pia kina mama wanaopitia wakati mgumu wapate usaidizi wa kifedha - na kupendekeza kwamba kila mwenye mtoto atapata madola ya mamilioni.
"Kile kinachoweza kutuweka huru ni kuheshimu sheria tulizowekewa na waanzilishi wa taifa hili," alisema. "uavyaji mimba unastahili kuruhusiwa kisheria kwasababu unajua nini? Sheria hiyo sio ya Mungu, kwa hiyo uhalali wake uko wapi?"
Wakati mwingine alionekana kutoa hotuba ambayo haikutarajiwa ya karne ya 19 kuhusu mwanahakati aliyependelea uavyaji mimba Harriet Tubman.
Tubman alizaliwa katika utumwa, lakini alifanikiwa kutoroka mashamba ya Maryland 1849 akiwa na umri wa miaka 27. Kisha alirejea Kusini kunusuru watumwa wengine na kuhatarisha maisha yake mwenyewe kuongoza wengine katika upatikanaji wa uhuru.
West pia alibubujikwa na machozi alipozungumza kuhusu marehemu mama yake aliyekufa 2007 baada ya upasuaji wa urembo kwenda mrama.


EmoticonEmoticon