Kenya Yatangaza Siku Tatu Za Maombolezo Ya Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa

Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametangaza kuwa Kenya itakuwa katika maombolezo ya siku tatu baada ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania, Benjamin William Mkapa.
Maombolezo hayo kitaifa yatakuwa kuanzia siku ya Jumatatu mpaka Jumatano.
Bendera nchini humo na ya Afrika Mashariki zitapepea nusu mlingoti kwa siku tatu za maombolezo.
Benjamin Mkapa alikuwa na mchango mkubwa kwa Kenya katika masuala mbalimbali hasa ya kidiplomasia, akiwa mmoja kati ya watu muhimu walioshiriki mchakato wa kupatikana kwa amani nchini Kenya wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi wa Kenya za mwaka 2008.


EmoticonEmoticon