Makamu Wa Rais Akutwa Na Corona Gambia

Isatou Touray
Makamu wa Rais wa Gambia, Isatou Touray amekutwa na maambukizi ya COVID19 na kutokana na hilo, Rais Adama Barrow atajitenga kwa muda wa siku 14.

Bi Touray (65) ambaye alitangazwa kuwa Makamu wa Rais wa nchi hiyo mwaka jana alisema yuko katika hali nzuri na ataenda karantini. Ikulu ya Gambia iliandika katika ukurasa wake wa Twitter.

Gambia imerekodi jumla ya visa 326 na vifo 9 vya Corona Virus, idadi ambayo ni ndogo zaidi kuripotiwa kwa ukanda wa Afrika Magharibi.


EmoticonEmoticon