Marekani Yaiamuru China Kufunga Ubalozi Wake

Ubalozi
Marekani imeiamuru China ifunge ubalozi wake mdogo uliopo mjini Houston, Texas, kufikia Ijumaa, hatua iliyoelezewa kama "uchokozi wa kisiasa " na Beijing.
Wizara ya mambo ya nje ya Marekani imesema kuwa uamuzi huo unalenga "kulinda akilimiliki ya Wamarekani ".
Lakini msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje ya Uchina Wang Wenbin amesema kuwa uamuzi huo "ni wa kushitua na usio na sababu ".
Taarifa hii imekuja baada ya watu wasiojulikana kuchukuliwa video wakichoma karatasi katika pipa la taka katika eneo la jingo.
Hali ya wasiwasi imekua ikiendelea kuongezeka baina ya Marekani na China kwa muda.


EmoticonEmoticon