Mike Pompeo Kuhojiwa Na Bunge La Marekani

Wabunge wa Marekani wanatarajiwa kumhoji Waziri wa Mambo ya Kigeni Mike Pompeo kuhusiana na Nchi hiyo inavyoshughulika na China na Urusi, uamuzi wa kuhamisha Wanajeshi kutoka Ujerumani na mauzo ya silaha, wakati mwanadiplomasia huyo wa juu atakapotoa ushahidi mbele ya Baraza la Seneti .

Pompeo atatoa ushahidi katika kikao cha kamati ya uhusiano wa nje kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miezi 15, kujadili maombi ya bajeti ya kila mwaka ya Wizara yake.

Wajumbe wa kamati ya uhusiano wa nje kutoka chama cha Democratic walitoa ripoti wiki hii ambayo imekosoa vikali muhula wa Pompeo Wizaranj hapo, ikisema amedhoofisha uwezo wa Wizara hiyo kuendesha diplomasia kwa kuacha wazi nafasi za kazi kwa miezi kadhaa, kuwatendea vibaya wanadiplomasia na kukuza utamaduni wa kulipa kisasi.

Wabunge wanatazamiwa pia kumuuliza Pompeo kuhusu hatua ya rais Donald Trump, kumfuta kazi kwa ghafla mwezi Mei, Steve Linick, mkaguzi mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje, wakati akichunguza mauzo ya silaha kwa Saudi Arabia.


EmoticonEmoticon