Msichana Wa Miaka 12 Aozeshwa Kwa Wanaume 2 Ndani Ya Kipindi Cha Mwezi Mmoja

Msichana wa miaka 12 ameokolewa nchini Kenya na mamlaka baada ya kuozwa wanaume wawili katika kipindi cha mwezi mmoja.

Babake msichana huyo anayeishi katika kaunti ya Narok iliopo magharibi mwa mji mkuu wa Nairobi alimlazimisha kufunga ndoa na mwanamume mwenye umri wa miaka 51.
Alitoroka na baadaye kuozwa mwananume mwengine mwenye umri wa miaka 35 kabla ya kuokolewa na maafisa wa haki za watoto na maafisa wa serikali.
Nchini Kenya kufunga ndoa na mtu aliye chini ya umri wa miaka 18 ni uhalifu.
Mwanaharakati wa haki za watoto alisema kwamba alipashwa habari kuhusu msichana huyo wakati alipokuwa katika harakati za kumuokoa msichana mwengine.
Babake alimuoza kwa mzee huyo, hivyobasi hakuwa na chaguo bali kuolewa na kijana huyo, Joshua Kaputah kutoka kwa shirika la Muungano wa amani Narok aliambia BBC.
Bwana Kaputah aliongezea kwamba ufukara na kufungwa kwa shule kutokana na mlipuko wa virusi vya corona umesababisha ongezeko la visa vya ndoa za watoto.
''Baadhi ya familia zinakabiliwa na njaa na uwezekano wa kupokea ng'ombe mbili au tatu za mahari unawavutia wengi'', alisema.
Credit: Bbc


EmoticonEmoticon