Naomba nichukue walau dakika zako chache niweze
kukueleza kinagaubaga ni kwa jinsi gani unaweza kupunguza mwili wako kwa
kutumia hatua zifuatavyo:
1. Zingatia
muda wa kula.
Watalamu wa masuala ya afya wanasema muda mzuri wa kula
chakula ni masaa manne baada ya kuamka, pia chakula cha mchana kiliwe tena
baada ya masaa nne mara baada ya kupata kifungua kinywa, na masaa takribani
matatu kabla ya kulala, kufanya hivi huupa mwili wako mda wa kukimen’genya
chakula vizuri na kuyeyusha mafuta yaliyopo kwenye chakula pia.
Hivyo
unakumbushwa kufanya hivi kila wakati kama kweli unataka kupunguza mwili wako.
2. Epukana
msongo wa mawazo
Msongo wa mawazo au stress hupelekea kula vyakula ambavyo
sio sahihi kwa afya yako na kwa wingi kama vile pombe, snacks mfano crips,
biskuti, pipi,c hocolate na kadhalika hata hivyo mwili huhifadhi mafuta kwa
wingi kipindi ukiwa na stress, hivyo kila wakati epuka kula vyakula ambavyo
vitakusababishaia kuwa mwili wenye mafuta.
3. Kutoruka
mlo wa asubuhi(breakfast)
Wengi wetu tumejikuta tukimaintain kwa kuruka breakfast na
baadae kujikuta tukifidia ule mlo kwa kula chakula kingi zaidi, Kufanya hivi
sio kujipunguza bali kukufanya uzidi kunenepa zaidi, hivyo unatakiwa kuzingatia
ya kwamba hauli chakula kingi kama mchana hukupata kifungua kinywa,
unachotakiwa kufanya ni kula chakula cha kawaida tu.
4. Angalia
aina ya chakula.
Aina ya vyakula sahihi tunavyopaswa kula ni vyakula vyenye
protein kwa wingi kama vile mboga za majani na matunda kwa wingi pia ,wanga
kidogo bila kusahau unywaji maji ya kutosha. Kufanya hivi kutakusaidia kuweza
kupungua na kuwa na mwili wa kawaida.
5. kupata
usingizi wa kutosha
Inashauriwa kulala masaa 6 hadi 8, kwani Kutopata usingizi
wa kutosha hufanya mwili wako kumen’genya chakula taratibu .
Lakini pia diet tu haitoshi mazoezi nayo ni muhimu katika
kupunguza uzito,hakikisha unafanya mazoezi walau mara tatu hadi nne kwa week
kwa muda wa dakika 20 hadi 30.
EmoticonEmoticon