Raisi Wa Kenya Apiga Marufuku Uuzaji Wa Pombe Nchini Humo

Uhuru Kenyatta
Hakutakuwa na uuzaji wa pombe katika migahawa na maeneo ya kuuza vyakula kwa kipindi cha siku 30 zijazo, amesema rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Rais Kenyatta amesema kwamba baa zote zitafungwa mara moja akiongezea kwamba zile ambazo zitakiuka agizo hilo jipya zitapokonywa leseni zao.
"Baa zitakazokiuka agizo hilo zitapokonywa leseni zao'' , alisema Uhuru.
''Masharti yote ambayo ninayatangaza yataheshimiwa na Wakenya wote bila kujali nyadhfa zao katika jamii'', aliongezea.
Aidha rais Uhuru Kenyatta amesema kwamba marufuku ya kutotoka nje kuanzia saa tatu usiku hadi saa kumi na moja alfajiri itaendelea kuwepo kwa kipindi chengine cha siku 30.
Amewataka Wakenya kufutilia mbali dhana potofu kwamba viwango vya chini vya vifo vina maana kwamba ugonjwa jhio sio hatari.
''Tatizo letu ni kuongezeka kwa wagonjwa wanaoambukizwa virui hivi na katika maeneo kwa mfano kama nairobi ugonjwa huu umeongezeka sana ,vijana wamekuwa wakiwaambukiza wazazi wao'' ,alisema.
Amesema kwamba vitendo vya hatari vinavyotekelezwa na vijana wakati huu vimehatarisha maisha ya wengine katika jamii.
Ongezeko la wagonjwa wa covid-19 linajiri baada ya hotuba yake ya tarehe 6 mwezi Julai ambapo aliondoa baadhi ya masharti ikiwemo kuruhusu watu kutoka katika kaunti zilizotajwa kuwa na maambukizi ya juu kama vile Nairobi, Mandera na Mombasa kusafiri.
Tatizo limekuwepo katika udhabiti wa kiuchumi huku mashirika mengi yakiwafuta kazi watu wengin na wengine wakipunguza mishahara ya wafanyakazi wao mbali na wafanyabiashara kukadiria hasara kubwa kutokana na marufuku ya mikusanyiko ya watu.
Kaunti 44 kati ya 47 tayari zimeripoti maambukizi ya virusi vya corona .
Ni kaunti ya Baringo , ile ya Pokot magharibi na ile ya Mandera ambazo hazijawahi kuripoti mgonjwa wa corona.


EmoticonEmoticon