Raisi Wa Marekani Asitishia Kuwapeleka Wanajeshi Katika Miji Zaidi Ya Marekani

Donald Trump
Rais Donald Trump ametishia kutuma maafisa wa jeshi katika miji mingi zaidi Marekani kudhibiti maandamano yanayoendelea.

Bwana Trump Jumatatu amekosoa miji kadhaa inayoongozwa na chama cha "liberal Democrats'', ikiwemo Chicago na New York, akisema kuwa viongozi wanaogopa kuchukua hatua.
Alisema kuwa maafisa waliotumwa Oregon wamefanya kazi nzuri ya kurejesha amani huku kukiwa na siku kadhaa za maadhamano eneo la Portland.
Hata hivyo, maafisa wa eneo wamesema kuwa maafisa wa serikali wanafanya hali kuwa mbaya zaidi.
Akizungumza katika Ikulu ya Marekani Jumatatu, Bwana Trump alirejelea wito wa utekelezaji sheria na utaratibu.
"Tunatuma vikosi," aliwaambia wanahabari. "Hatuwezi kuacha hili liendelee kutokea katika miji."
Alitaja miji ya New York, Chicago, Philadelphia, Detroit, Baltimore na Oakland akiwa anazungumzia matatizo yatokanayo na ghasia.
"Hatuwezi kuacha hili litokee katika nchi yetu, yote ni maeneo yanayoongozwa na chama cha liberal Democrats."
Viongozi wa majimbo wametaka Bwana Trump kuondoa maafisa alioagiza kupelekwa huko Portland na kumshutumu kwa kufanya hali kuwa mbaya zaidi kama njia ya kutafuta ushawishi wa kisiasa mwaka wa uchaguzi.


EmoticonEmoticon