Raisi Wa Marekani Atetea Dawa Ya hydroxychloroquine Kwamba Inatibu Corona Huku Mamlaka Zikiwa Tayari Zimeonya Kuhusiana Na Dawa Hiyo

Donald Trump
Rais wa Marekani, Donald Trump kwa mara nyingine ametetea matumizi ya hydroxychloroquine kupambana na virusi vya corona, akiwachanganya maafisa wake wa afya.

Amedai kuwa dawa hiyo ya kutibu malaria ilikataliwa kutibu Covid- 19 kwa kuwa tu yeye ndiye aliyeipendekeza.
Kauli yake imekuja baada ya Twitter kumfungia mtoto wake mkubwa kwa kuchapisha taarifa kuhusu kutumia hydroxychloroquine.
Hakuna ushahidi kuwa dawa hiyo inaweza kupambana na virusi na wadhibiti wa dawa wanatahadharisha kuwa inaweza kusababisha matatizo ya moyo.
Mwezi uliopita, mamlaka ya chakula na dawa nchini Marekani (FDA) ilitahadharisha kuhusu matumizi ya dawa kwa ajili ya tiba ya virusi vya corona, baada ya ripoti kuhusu ''matatizo makubwa ya moyo'' na masuala mengine ya kiafya.
Mamlaka hiyo ilisitisha matumizi ya dharura ya dawa hiyo kutibu Covid-19. Shirika la afya duniani (WHO) limesema kuwa ''mpaka sasa hakuna ushahidi'' kuwa dawa hiyo ina ufanisi kutibu au kuzuia virusi vya corona.


EmoticonEmoticon