Raisi Wa Marekani Awataka Wananchi Wavae Barakoa

Donald Trump
Idadi ya maambukizi ya virusi vya corona imepindukia milioni 13 na vifo vilivyotokana na virusi hivyo ni zaidi ya laki sita kote duniani wakati ambapo wanasayansi wako mbioni kutafuta chanjo.

Kwa sasa baadhi ya chanjo zilizobuniwa ziko katika hatua ya majaribio kwa binadamu.
Tukianzia Marekani, Rais Donald Trump ameubadili msimamo wake kuhusiana na uvaaji wa barakoa na sasa anawataka Wamarekani wazivae kila wanapokuwa katika mikusanyiko. 
Katika kikao chake cha kwanza na waandishi wa habari cha kuzungumzia hali ya virusi vya corona Marekani baada ya miezi kadhaa, Trump ameonya kwamba kabla maambukizi kupungua nchini humo, hali itakuwa mbaya zaidi.
"Nitaivaa nikiwa kwenye kundi la watu, nikiwa na walinzi wangu nataka kuwalinda pia kwa hiyo nitavaa barakoa, sina tatizo na barakoa. 
Mtazamo wangu ni huu, kitu chochote kinachoweza kusaidia na bila shaka barakoa inaweza kusaidia, ni kitu kizuri. Sina shida, ninaibeba, ninaivaa, mumeniona nikiivaa mara kadhaa na nitaendelea," alisema Trump.


EmoticonEmoticon