Ripoti Zimesema Ndege Za Kivita Za Marekani Zilikuja Karibu Sana Na Ndege Ya Abiria Ya Iran Nchini Syria

Iran nchini Syria
Vyombo vya habari vya Iran' vimesema ndege za kivita za Marekani zilikuja karibu sana na ndege ya abiria ya Iran nchini Syria - lakini madai hayo yamekanushwa na Marekani.

Televisheni ya taifa ya Iran, Irib imesema rubani wa ndege ya Mahan alibadilisha muelekeo haraka , jambo ambalo lilisababisha abiria kadhaa kujeruiwa.
Video ambayo iliwekwa kwenye televisheni ya Irib inaonyesha ndege moja ya kivita kupitia dirisha la ndege na abiria mmoja akiwa anachirizika damu.
Lakini jeshi la Marekani baadae lilisema ndege nambari F-15 ilikuwa katika umbali salama.
"Ndege ya Marekani F-15 ilikuwa katika misheni yake ya kawaida katika anga la eneo la [al]-Tanf nchini Syria, na ndege ya abiria ya Mahan ilikuwa katika umbali salama wa takribani mita 1,000 [maili 0.6 ] kutoka kwa ndege yao majira ya jioni," Kapteni Bill Urban, msemaji wa Marekani alitoa maelezo hayo jioni ya Alhamisi.
Alisema ukaguzi ulifanyika kuhakikisha usalama wa watu katika kambi za jeshi za Marekani huko al-Tanf, karibu na mpaka wa Iran na Jordan.
"Kwanza rubani wa F-15 alibaini kuwa ndege ya abiria ya Mahan A F-15 ilikuwa katika umbali salama,"aliongeza.
Ndege ya Mahan ilibidi kuhairisha safari na kutoka Tehran kwenda Beirut na kutua salama katika mji mkuu wa Lebanese.
Haikujulikana kwa haraka kuwa ndege hiyo ilikuwa na abiria wangapi na wafanyakazi wa ngapi wa ndege.
Baada ya ndege hiyo kujaza mafuta , iliruka kurejea mji mkuu wa Iran, siku ya Ijumaa.
Ripoti za awali kutoka chombo cha habari cha Irib, kilisema ndege mbili za kivita zinaweza kuwa za Israeli.
Aidha Israel nayo ilikanusha kuhusika na tukio hilo.


EmoticonEmoticon