Ripoti Zinasema Janga La Corona Litaporomosha Uchumi Wa Nchi Za Kiarabu

Ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo imesema kuwa janga la virusi vya corona litasababisha hasara kubwa kwa mataifa ya kiarabu na kusababisha kuporomoka kwa uchumi kwa asilimia 5.7 mwaka huu hali itakayosababisha umaskini kwa mamilioni ya watu na kuongeza mateso kwa wale walioathirika kutokana na ghasia. 

Tume ya uchumi na masuala ya kijamii ya Umoja wa Mataifa ya eneo la Magharibi mwa bara Asia, inatarajia chumi za baadhi ya mataifa ya bara Asia kuporomoka kwa hadi asimia 13 na kusababisha hasara jumla kwa eneo hilo ya dola bilioni 152. 

Ripoti hiyo imesema kuwa watu wengine milioni 14.3 wanatarajiwa kuingia katika hali ya umaskini na kuongeza idadi jumla kufikia milioni 115 hii ikiwa ni robo ya idadi kamili ya watu katika mataifa ya kiarabu. 

Zaidi ya watu milioni 55 katika eneo hilo walikuwa wanategemea msaada wa kibinadamu kabla ya janga la virusi vya corona ikiwa ni pamoja na watu milioni 26 waliolazimika kuyahama makazi yao.


EmoticonEmoticon