Sababu 6 Za Kwanini Wanawake Huishi Miaka Mingi Zaidi Ya Wanaume

Uzee
Mara nyingi tumeshuhudia katika familia nyingi mwanaume akitangulia kufa kabla ya mwanamke. Simaanishi kuwa wanaume wote wanakufa mapema, lakini mara nyingi wanawake huishi zaidi kuliko wanaume.

Utafiti zaidi juu ya sababu za wanaume wengi kufa mapema kuliko wanawake.

1. Wanawake hujali afya zao zaidi
Tafiti mbalimbali zilizofanywa na wataalamu wa afya zilibaini kuwa wanawake hujali afya zao zaidi. Tafiti hizo zinaeleza kuwa wanawake wengi wanapojihisi kuumwa huenda hosipitalini ili kupata ushauri wa kitaalamu.

2. Wanaume huendeleza tabia hatarishi zaidi
Tabia kama vile uvutaji wa sigara, pombe au madawa ya kulevya mara nyingi hufanywa na wanaume. Hili limepelekea kuathiri afya zao kwa kiasi kikubwa na kusababisha kufupisha maisha ya wanaume wengi.

3. Wanaume hujiua zaidi kuliko wanawake
Takwimu mbalimbali zinaonyesha kuwa kiwango cha vifo vinavyotokana na kujiua kwa wanaume ni kikubwa kuliko kwa wanawake.

4. Wanawake wanapenda kushirikisha watu wengine
Kuna usemi usemao “mwanaume ana kifua cha kutunza mambo”; kwa hakika kwa upande mwingine hili ndilo huchangia wanaume kufa mapema.

5. Maradhi ya moyo huchelewa kutokea kwa wanawake
Tafiti zilizofanywa huko Marekani, zilibaini kuwa maradhi ya moyo huua wanaume na wanawake lakini maradhi haya huchelewa kwa takriban miaka 10 kwa mwanamke.

6. Kazi wanazofanya wanaume zinawachakaza
Naamini swala la kazi ngumu au hatari kwa wanaume linafahamika wazi, wanaume hufanya shughuli za shuruba bila hata kupumzika au kula vyema.

Kwa hakika uhai wa mtu uko mikononi mwa MUNGU, lakini kuna badhii ya mambo huchangia kufupisha uhai wa mtu. Ikiwa wewe ni mwanaume na unaweza kuyaepuka badhii ya mambo yaliyoelezwa hapa, basi fanya hivyo ili angalau uongeze siku kadhaa.


EmoticonEmoticon